Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, maandamano yalianza mbele ya Duomo mjini Milan, mahali ambapo washiriki wa maandamano walionesha bango lenye urefu wa mita 27 (futi 99), ambalo lilikuwa limeandikwa majina ya watoto 18,457 wa Palestina waliouawa huko Gaza kati ya tarehe 7 Oktoba 2023 na 31 Julai 2025.
Kabla ya kufunuliwa kwa bango hilo, waandamanaji walisimama kimya katika uwanja huo, ikiwa ni hatua ya kupinga mauaji na uhalifu wa utawala wa Kizayuni; kisha waliinua bendera za Palestina na shali ili vionekane katika umati wote wa watu.
Waandaaji wa maandamano walielezea kitambaa hicho kama alama ya watoto waliouawa wakati wa vita vinavyoendelea.
Washiriki walibeba kitambaa cheupe kilichokuwa ni ishara ya sanda kubwa kutoka Uwanja wa Kanisa Kuu kuelekea Ngome ya Sforzesco katika maandamano ya kimya kwa ajili ya kuwaenzi wahanga na kupinga ukaliaji pamoja na mauaji yanayofanywa na wanajeshi wa Israel huko Ghaza.
Kuhusu takwimu zilizotajwa katika matini hiyo, imeelezwa kwamba; tangu Oktoba 2023, kwa mujibu wa takwimu za Palestina, karibu Wapalestina 73,000 wameuawa na zaidi ya watu 173,000 wamejeruhiwa, ambapo wengi wao ni wanawake na watoto.
Chanzo: Shirika la Habari la Anadolu.
Maoni yako